
Vijana Wana-Ekaristia
URAFIKI NA YESUMAISHA NA YESUUSHIRIKA NA YESU
Marafiki Katika Meza Ya Kristo
URAFIKI NA YESU
Moyo wa Wana Ekaristia ni urafiki na Yesu. Wanajitahidi kujua mapenzi ya Mungu kupitia mafundisho ya Yesu katika Injili.
MAISHA NA YESU
Moyo wa Wana Ekaristia ni kuishi urafiki huu, wakipata lishe na mfano katika Ekaristi Takatifu. Ekaristi huwapa vijana wa utume huu nguvu ya kuyaishi mapenzi ya Mungu na mfano wa kujisadaka.
USHIRIKA NA YESU
Moyo wa Wana Ekaristia ni kushiriki maisha na utume wa Yesu kama Kanisa, kutumikia haki ya Ufalme wa Mungu. Humshuhudia Kristo pale walipo kwa kuyaishi maadili ya Kikristo na kuruhusu Yesu kutumia maisha yao katika utume wa upendo na ukombozi.
