RMOP Tanzania Logo

Nia ya Sala ya Baba Mtakatifu

Kuunganisha Sala na matendo kukabili changamoto za wanadamu na utume wa Kanisa

Kila mwezi · Pamoja na Papa · Sauti Moja · Ulimwenguni Pote

Nia ya Sala

Kila mwezi, Baba Mtakatifu anatoa nia ya Sala kwa Mtandao wake wa Sala Ulimwenguni. Nia hizi huonesha jinsi Kanisa analoliongoza linavyowajali sana wanadamu na Utume wa Kristo lililokabidhiwa. Nia hizi ni mwito kwa watu wote ulimwenguni kufanya matendo mema. Zinatuelekeza tunaosali kuziweka Sala zetu katika matendo yenye mguso chanya kwa maisha ya watu, na kuutazama ulimwengu kwa moyo wa huruma wa Kristo.

slider image

Tukisali pamoja na Mama Malkia wa Mitume

SALA YA MAJITOLEO YA KILA SIKU

Kuishi Kama Mitume wa Sala

Ushiriki wa Wazi

Uko wazi kwa kila mbatizwa. Inahusisha kuingiza Nia za Sala za Papa katika Sala za kila siku na kushiriki hasa Ijumaa ya Kwanza ya kila mwezi. Inaweza kufanywa na watu binafsi au vikundi kama wanakwaya, watumishi wa altare, wanafunzi, na jumuiya mbalimbali.

Uanachama wa Utume

Ni njia ya kina zaidi kwa kuanzisha uhusiano na ofisi husika. Inajumuisha malezi, mikutano, mafungo na kufuatilia taarifa rasmi. Inaweza kuwa ya mtu binafsi au ya kikundi/jumuiya yenye muundo wa kitume.

Mtu Binafsi

Kuishi nyakati tatu za Sala kila siku: Asubuhi (Sala ya kujitoa), Mchana, na Usiku. Lengo ni kukua katika urafiki wa karibu na Bwana, kwa pamoja na Mama Maria.

Kikundi/Jumuiya

Jumuiya za parokia, shule, vyuo au vikundi vya kitume hushiriki Sala, malezi, mafungo na matendo ya huruma; pia huunga mkono Vijana Wana-Ekaristia (EYM).

Wakfu Binafsi

Kwa wenye wito wa ukaribu na Moyo Mtakatifu wa Yesu. Hufanya agano rasmi na Kanisa, wakijiweka tayari kuhudumia familia ya Mtandao wa Sala na EYM.

Nia ya Sala

Ungana nasi kwa kusoma au kudownload Nia ya Sala