RMOP Tanzania Logo

Mtandao wa Sala wa Baba Mtakatifu Ulimwenguni

(Zamani Uliitwa Utume wa Sala)

Ushirika wa Kipapa unaowaunganisha Wakatoliki kote duniani kukabili changamoto za wanadamu na za utume wa Kanisa kwa njia ya Sala na matendo mema. Changamoto hizi hutolewa kila mwezi kwa Kanisa lote kupitia Nia za Sala za Baba Mtakatifu. Kila Mkristo anaalikwa kuziombea na kuziishi kwa vitendo katika maisha ya kila siku, akichangia kuujenga ulimwengu wa matumaini, huruma, na mshikamano.

Chimbuko

Mtandao wa Sala wa Baba Mtakatifu ulianzishwa mwaka 1884 kama “Utume wa Sala”. Ulizaliwa kutokana na hamu ya waamini kushiriki kazi ya kimisionari, hata wale ambao hawangeweza kusafiri mbali. Suluhisho likawa ni kushiriki utume huo kwa njia ya Sala na kwa kuuishi vema Ukristo wao katika maisha ya kila siku.

Leo, utume huu upo katika nchi 92 na unaunganisha zaidi ya Wakatoliki milioni 22, ukiwajumuisha pia vijana kupitia tawi la Vijana Wana-Ekaristia (EYM).

Ulimwengu Mmoja

Kutoka 1884 hadi leo, Mtandao wa Sala umekuwa daraja linalowaunganisha waamini duniani kote kuwa sauti moja ya Sala, mioyo iliyounganishwa kwa ajili ya Kristo na ulimwengu.

Jukumu Letu

Kutumia Sala na matendo mema kama njia ya kukabiliana na changamoto za wanadamu na za utume wa Kanisa.

Lengo Letu

Kuchangia katika kuutakatifuza ulimwengu kwa kuzisali na kuziishi nia za Sala za Baba Mtakatifu.

Utume Wetu

Kuwa mitume wa Kristo katika maisha ya kila siku kupitia “Njia ya Moyo” – njia ya huruma kwa ulimwengu.